<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><title>Mapenzi Yako Yafanyike, Bwana TZR91</title>
<lyrics>[V1]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Wewe mfinyanzi, nami towe,
 Unifinyange upendavyo,
 Mimi tayari, naja kwako.

[V2]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Unihoji dhambi zote,
 Unisafishe vya kimwili,
 Niinamapo Msalabani.

[V3]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Mimi dhaifu, mimi mnyonge.
 Uwezo wote, kwako kweli,
 Sasa niponye, Ee, Mwokozi.

[V4]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Natoa kwako vitu vyote,
 Maisha, mali, moyo, mwili,
 Vyote ni vyako, kweli, kweli.

[V5]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Mapenzi yangu yavunjike,
 Ninakubali uwe Bwana,
 Ni mali yako, twaa kabisa.

[V6]
 Mapenzi yako yafanyike,
 Unitawale siku zote,
 Sura ya Yesu umba kwangu,
 Nijaze Roho nayo nguvu.</lyrics>
<hymn_number>91</hymn_number>
</song>